Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaonya kuhusu matumizi ya njia zisizofaa katika kutambua ugonjwa wa Kifua kikuu

WHO yaonya kuhusu matumizi ya njia zisizofaa katika kutambua ugonjwa wa Kifua kikuu

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa kutumika kwa damu katika kutambua ugonjwa wa kifua kikuu mara nyingi huwa matokeo yasiyo ya ukweli na kusababisha madhara kwa afya ya umma. Sasa WHO inazishauri nchi kupiga marufuku kupimwa kwa damu kusikoidhinishwa.

WHO inasema kuwa kupimwa kwa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kutumia chechembe za kukinga ni suala gumu na huenda hata wakati mwingine ikaonyesha wasiokuwa na ugonjwa wa kifua kikuu kuwa na ugonjwa huo. Daktari Mario Raviglione ni mkurugenzi kwenye idara ya kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu kwenye shirika la WHO.