Bendera ya Sudan Kusini ya pepea kwenye Umoja wa Mataifa

14 Julai 2011

Bendera ya taifa la Sudan Kusini imepandishwa kwenye mlingoti kwenye sheria zilizokuwa na hisia nyingi zilizofanyika hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na kuwa taifa la 193 kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Makamu wa rais nchini Sudan Kusini Riek Machar Teny ameitaja siku hii kama siku muhimu kwa nchi yake. Kila rangi kwenye bendera ya Sudan inawakilisha suala tofauti kwa mfano rangi nyeusi inawakilisha wananchi, nyeupe inawakilisha amani, nyekundu inawakilisha damu iliyomwagika , kijani inawakilisha ardhi na ya samawati ikiwakilisha mto Nile. Nyota inawakilisha umoja ya majimbo ya taifa hilo jipya.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter