Baraza la Usalama waikosoa Syria kutokana na kushambuliwa kwa balozi kadhaa.

13 Julai 2011

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa pamoja na Baraza la Usalama amelaani vikali tukio la mashambulizi katika ofisi za ubalozi huko Damasca Syria ambako kumesababisha kuwepo kwa uharibifu pamoja na kuwajeruhiwa wanadiplomasia kadhaa.Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, balozi za Marekani na Ufaransa nchini humo ndizo zilizoshambuliwa katika tukio hilo.

Wakati Ban akisisitiza wito wa kutaka kuanza kwa mchakato wa majadiliano ili kukaribisha mabadiliko ya kisasa, Baraza la Usalama limelaani tukio la mashambulizi hayo na kuongeza kuwa linakwenda kinyume na misingi ya uheshimuji wa mamlaka za kidiplomasia.Baraza hilo la usalama limeitaka mamlaka za Syria kutoa ulinzi kwa ofisi za kibalozi pamoja na watumishi wake.Kwa kipindi cha miezi kadhaa sasa, Syria inashuhudia hali mbaya ya kisasa na kuendelea kushamiri kwa maandamano kunazidi kuiweka majaribuni serikali ya nchi hiyo ambayo waandamanaji wanataka iondoke.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter