Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaripoti mkurupuko wa Kipindupindu na Surua nchini DRC

WHO yaripoti mkurupuko wa Kipindupindu na Surua nchini DRC

Shirika la afya duniani WHO limeripoti mkurukupo wa ugonjwa wa surua na kipindupindu kwenye Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo zaidi ya watu 2,500 wameaga dunia.WHO inasema kuwa jitihada za kukabiliana na magonjwa hayo kwa njia ya chanjo na usambazaji wa bidhaa za usafi zimetatizwa na ukosefu wa fedha.

Ugonjwa wa surua unaripotiwa kusambaa kwenye mikoa saba mashariki mwa DRC huku ule wa kipundupindu ukiripotiwa kwenye mkoa wa Kisangani ambapo umesambaa hadi mjini Kinshasa ukipitia mto Congo. Tarik Jasarevic kutoka WHO anasema kuwa kwa sasa dola milioni 9 zinahitajika kugharamia kampeni za chanjo ili kuweza kukabilina na ugonjwa wa Surua.

(SAUTI YA TARIK JASAREVIC)