Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR yapinga dhuluma zinazoendeshwa nchini Malaysia

OHCHR yapinga dhuluma zinazoendeshwa nchini Malaysia

Afisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHC inasema kuwa imekuwa ikipokea ripoti za dhuluma ambazo zimekuwa zikiendeshwa na serikali ya Malaysia zikiwemo za kukamatwa, kupigwa na vitisho dhidi ya wanachama wa vuguvugu lijukanalo kama (Coalition for Clean and Fair Elections) linapojiandaa kuongoza maandamano ya amani yanayotarajiwa kufanyika tarehe 9 mwezi huu.

Kulingana na ripoti takriban watu 150 wamekamatwa au kushtakiwa wakiwemo wanachama wa upinzani bungeni. Kwa sasa ofisi ya tume ya haki za binafdamu ya Umoja wa Mataifa inatoa wito kwa utawala kuwaachilia huru wote wanaozuiliwa kwa kuwa wana haki ya kujieleza .