Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

China imevunja makubalino ya kimataifa ya kupambana na ukwepaji wa sheria

China imevunja makubalino ya kimataifa ya kupambana na ukwepaji wa sheria

China imeshutumiwa kwa kumualika rais wa Sudan Omar El Bashir na kushindwa kumkamata kulingana na waranti uliotangazwa dhidi yake na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa kwa kushindwa kumkamata rais Bashir, China imekiuka makubaliono ya kimataifa ya kupambana na ukwepaji wa sheria na katika kuwafikisha mbele ya sheria wanaoshutumia kwa kutenda uhalifu dhidi ya ubinadamu. Akiongea mjini Geneva Bi Pillay amesema kuwa China inaweza kutenda zaidi katika kuunga mkono haki za binadamu kote duniani zikiwemo nchi zilizo na uhusinao wa kibiashara.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)