Vyandarua milioni 190 vilivyotibiwa vya kuzuia Malaria vyasambazwa

28 Juni 2011

Mfuko wa kimataifa wa kusaidia kupambana na ugonjwa wa Malaria na HIV unasema kuwa zaidi ya vyandarua milioni 190 vya kuzia mbu vilivyotibiwa vimesambazwa kwa familia tangu mwaka 2003. Kati ya vyandarua hivi, vyandarua milioni 70 vimesambazwa kwa muda wa miezi 12 iliyopita. Pia huduma milioni 36 za unyunyizaji wa dawa ya kuua mbu zilitolewa ikiwa ni ongezeko la asilimia 31 tangu mwaka mmoja uliopita.

Wakati huohuo kwa muda wa miezi 12 iliyopita watu 400 wanaoishi na virusi vya Ukimwi walianza kutumia madawa ya ARVS. Pia watu milioni 1.2 wamepata matibabu ya ugonjwa wa Kifua kikuu hali ambayo imepunguza vifo vinavyosababishwa na ugojwa wa Malaria na Ukimwi. Daniel Low Beeer ni Mkurugenzi wa utendaji wa mfuko wa kimatifa wa kusaidia kupambana na ugonjwa wa Malaria na HIV.

(SAUTI YA DANIEL LOW BEEER)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter