Mkutano wa UM kwa amani kati ya Israel na Palestina wang’oa nanga mjini Brussels

28 Juni 2011

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kuunga mkono mpango wa amani kati ya Israel na utawala wa Palestina umeng’oa nanga hii leo mjini Brussels ukiwa na kauli mbiu “Wajibu wa Ulaya katika kupatikana kwa taifa la Palestina na kuleta amani kati ya Waisrael na Wapalestina.”

Mkutano huo utakuwa na lengo la kuchangia kwenye jitihada za kimataifa za kuleta amani kati ya Israel na utawala wa Palestina kwa kungalia zaidi ni wajibu upi ulaya inaweza kuchukua.Wanaotarajiwa kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Abdou Salam Diallo mwenyekiti wa kamati inayohusika na haki za wapalestina pamoja na Maxwell Gaylard ambaye ni naibu mratibu kwenye mpango wa amani wa mashariki ya kati.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter