Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fanya kitu kimoja, jifunze, fikisha ujumbe na toa msaada kunusuru wakimbizi

Fanya kitu kimoja, jifunze, fikisha ujumbe na toa msaada kunusuru wakimbizi

Jumatatu ijayo ni siku ya wakimbizi duniani ambapo ujumbe maalumu mwaka huu ni “fanya kitu kimoja, jifunze, fikisha ujumbe na toa msaada” kwani mkimbizi mmoja asiye na matumaini hao ni wakimbizi wengi. Kila siku mamilioni ya wakimbizi duniani wanakabiliwa na mauji, ubakaji na ugaidi dhidi ya maisha yao.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa wito kwa kila mmoja kuchukua hatua ili kusaidia kumaliza adha zinazowakabili wakimbizi hasa ukizingatia dunia hivi sasa inakabiliwa na changamoto na migogoro karibu kila kona kuanzia Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini, Afrika Magharibi na hata bara Ulaya.

UNHCR inaziomba nchi kuwa tayari kuwapokea na wahifadhi wakimbizi wanatafuta usalama wa maisha yao. Hata hivyo kuna baadhi ya nchi kama Burundi ambayo miaka ya nyuma ilikuwa moja mwa nchi zenye wakimbizi wengi duniani sasa hivi imepindua historia hiyo na kuanza kuwapa hifadhi wakimbizi .

Hadi sasa inahifadhi wakimbizi 43,000 kutoka Jamuhuri ya Kidemokarasia ya Congo na wakati huo huo UNHCR imeshawarejesha nyumbani maelfu ya wakimbizi wa Burundi kutoka Tanzania na kuwajengea nyumba zaidi ya laki moja ili kuanza maisha mapya.

Pamoja na hatua hiyo masuala ya wakimbizi bado yanakabiliwa na changamoto nyingi Burundi, kubwa likiwa ni ukosefu wa fedha za kutosha kukidhi mahitaji ya wakimbizi hao.

Kutoka Bujumbura , muandishi wetu Ramadhani KIBUGA amedhuru baadhi ya kambi za wakimbizi hao na kutuandalia makala hii, ungana naye kutoka Bujumbura.

(MAKALA NA RAMADHAN KIBUGA)