Mahiga akaribisha maafikiano baina ya Rais na spika wa bunge Somalia

9 Juni 2011

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Dr Augustine Mahiga ameelezea kuridhishwa kwake na makubaliano yaliyotiwa saini baina ya Rais wa Somalia Sheikh Sharif Sheikh Ahmed na spika wa bunge Sharif Hassan Sheikh Aden mjini Kampala chini ya uangalizi wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda na uwezeshaji wake.

Mahiga amesema ni mwelekeo mwema katika kutatua mzozo wa kisiasa unaoighubika Somalia kwa miezi mitano sasa, kuhusiana na kumaliza serikali ya mpito na mipango ya kisiasa ya baadaye. Kipindi cha serikali ya mpioto kinatarajiwa kumaliza mwezi Agosti na kuitishwa uchaguzi. Jason Nyakundi na taarifa zaidi

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter