Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone yawahukumu watu wanne

Mahakama ya uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone yawahukumu watu wanne

Mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa iliyobuniniwa kuwahukumu washukuwa wanaodaiwa kuhusika kwenye uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone imewahukumu watu watano kwa kuwahangaisha mashahidi waliotoa ushahidi kwenye kesi mbili.

Wawili kati ya washukiwa hao waliokuwa wanachama wa kundi la Armed Forces Revolutionary Council Ibrahim Bazzy Kamara na Santigie Borbor Kanu kwa sasa wanatumikia kifungo kwenye gereza na Mpanga nchini Rwanda kufuatia mashtaka ya uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone. Wengine ni Hassan Papa Bangura na Samuel Kargbo wanaoishi nchini Sierra Leone wanaokabiliwa na mashtaka ya kujaribu kuwahonga mashahidi