Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wa UM waliotekwa nyara Darfur waachiliwa

Wafanyakazi wa UM waliotekwa nyara Darfur waachiliwa

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mpango wa chakula WFP limeeleza kuwa wafanyakazi watatu wa kimataifa raia wa Bulgaria ambao walitekwa nyara huko Darfur nchini Sudan hatimaye wameachiliwa.

Wafanyakazi hao ambao waliokuwa chini ya WFP walitekwa nyara mwezi January mwaka huu wakati wakiwa kwenye operesheni za kawaida kwenye eneo hilo la Darfur ambalo bado linasongwa songwa na hali ya ukosefu wa usalama.

Ripoti zinasema wote watatu wako katika hali nzuri kiafya. Kuachiliwa huru wa wafanyakazi hao kunafuatia juhudi zilizoendeshwa na WFP

kushirikiana na serikali ya Sudan ambayo iliwashawishi vikundi vya waasi

vilivyoendesha utekaji nyara huo.

 Tukio hilo la utekaji nyara lilifanyika katika mji wa Um Shalaya,uliopo umbali

 wa kilometa 60 kutoka mji wa Darfur