Wahamiaji zaidi ya 200 hawajulikani waliko pwani ya Tunisia

3 Juni 2011

Duru za habari zinasema wahamiaji zaidi ya 200 hawajulikani waliko baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuharibika kwenye bahari ya Mediteraniani wakijaribu kuingia barani Ulaya.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tunisia , mabaharia wa Tunisia na jeshi la serikali wamewaokoa wahamiaji 500 lakini wengine 270 hawajapatikana na huenda wamezama wakaiti wakitapatapa kutaka kutoka nje ya boti hiyo kabla haijazama. Ili kupata taarifa zaidi idhaa hii imezungumza na Jumbe Omari Jumbe afisa mawasiliano na habari wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter