UM wataka uchunguzi dhidi ya mwandishi wa habari wa UN Venezuelan

2 Juni 2011

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na utetezi wa uhuru wa vyombo vya habari amelaani vikali tukio la mauwaji ya mwandishi mmoja wa habari nchini Venezuela ambaye aluwawa mwezi uliopita na ametaka mamlaka za dola kuwafuatilia wahusika wa tukio hilo.

Mwandishi huyo Wilfred Iván Ojeda ambaye alikuwa akiandika kwenye safu maalumu na pia alikuwa mwanavugugvu la demokrasia alikutwa ameuwawa kwa kupigwa risasi kwenye kichwani katika mji Victoria.

Kulingana na Mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la UNESCO Bi Irina Bokova wahusika wa tukio hilo lazima waletwe kwenye meza ya haki haki kwani wanazui na kubinya  uhuru wa mtu kujieleza na kutoa maoni yake.

Taarifa za vyombo vya habari zinasema kwamba mwandishi huyo alizingatia zaidi kuandika masuala ya kisiasa na hakuwa tishio kwa mamlaka zozote

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter