Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nafaka za dola bilioni 4 zinapotea Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara:FAO

Nafaka za dola bilioni 4 zinapotea Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara:FAO

Ripoti ya shirika la chakula na kilimo FAO na Bank ya dunia iliyotolewa leo inasema kuwekeza katika tekinolojia ya uhifadhi baaza ya mavuno itapunguza chakula kinachopotea au kuharibika na kuongeza usambazaji wa chakula Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.

Ripoti hiyo imetolewa kwenye mkutano ambao unahudhuriwa na wataalamu kutoka Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara mjini Roma Italia wakijadili jinsi ya kuhifadhi chakula kisipotee bure.

Ripoti hiyo iitwayo Missing Food, hali ya nafaka zinazopotea baada ya mavuno Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara iliyoandaliwa kwa ushirikiano na taasisi ya mali asili ya Uingereza inakadiria kwamba thamani ya nafaka zinazopotea baada ya mavuno ni takribani dola bilioni 4 kwa mwaka. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)