Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yawarejesha wakimbizi wa Liberia walio Ivory Coast

UNHCR yawarejesha wakimbizi wa Liberia walio Ivory Coast

Wiki hii shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeanza kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Liberia ambao wamekwama kwenye ofisi za shilika hilo mjini Abidjan Ivory Coast kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi.

Jumanne na Alhamisi ya wiki hii ndege mbikli zilisafirisha wakimbizi 264 hadi kwenye uwanja wa ndege wa Roberts kilometa 60 nje ya mji mkuu wa Liberia Monrovia.

UNHCR inasema wakimbizi hao ndio walioomba kurejeshwa nyumbani kwa hiyari yao. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)