Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya ICTY na UM wakaribishwa kukamatwa Mladić

Mahakama ya ICTY na UM wakaribishwa kukamatwa Mladić

Mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa ajili ya Yugoslavia ya zamani amekaribisha kukamatwa kwa Ratko Mladic hii leo. Mladic alikuwa generali na kamanda wa jeshi la jamhuri ya Serbia ya Bosnia na Herzegovina wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Alishitakiwa na mahakama hiyo Julai 25 mwaka 1995 kwa makosa ya uhalifu wa vita ikiwemo mauaji ya kimbari na amekuwa akikimbia mkono wa sheria kwa miaka 16 sasa.

Mwendesha mashitaka Barammertz (TAMKA BARAMEZ) amesema anakaribisha kukamatwa kwa Ratko Mladic nchini Serbia hii leo na mipango ya kumsafirisha kwenye kwenye mahakama hiyo inafanyika ili akabili mashitaka.

Ameshukuiru kazi iliyofanywa na serikali ya Serbia kumkamata na amesema wametimiza wajibu wao katika kutenda haki. Frederick Swinnen, ni mshauri wa mwendesha mashitaka katika mahakama ya ICTY

(SAUTI YA FREDERICK SWINNEN)

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon akizungumzia kukamatwa huko amesema hii ni siku ya kihitoria katika haki ya kimataifa, na amepongeza juhudi za serikali na Rais Tadic 9TAMKA TADICHI)wa Serbia .