Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama latoa muda kwa Somalia kuamua hatma yao

Baraza la usalama latoa muda kwa Somalia kuamua hatma yao

Ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa uliokuwa Nairobi Kenya kujadili suala la Somalia umekamilisha mkutano wake na kutoa muda wa serikali ya mpito kufanya maamuzi ya hatma yao.

Ujumbe huo umesema mkataba wa mani ya Somalia lazima utekelezwe na serikali ya mpito lazima imalize muda wake ili kutoa fursa ya demokrasia na amani kwa nchi hiyo iliyokuwa kwenye vita kwa zaidi ya miongo miwili sasa.

Mkutano wao uliofanyika Nairobi na kujumuisha pande zote husika ikiwemo serikali ya mpito, jimbo lililojitenga la Puntland na Galmadoug na wadau wengine umekamilika bila suluhisho la moja kwa moja lakini kwa kutoa muda wa wiki kadhaa kwa serikali ya mpito kuchukua hatia kama anavyofafanua mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Somalia Balozi Augustine Mahiga.

(SAUTI YA AUGUSTINE MAHIGA)