Ban awataka viongozi Somalia kuafikiana

26 Mei 2011

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezishauri idara za serikali ya mpito nchini Somalia kuonyesha kuwa zinaipeleka nchi hiyo mbele katika masuala ya kisiasa, kwenye maendeleo ya kijamii na kiuchumi akisema kuwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa na wafadhili wanapoteza uvumilivu kutokana na misukosuko kwenye uongozi.

Akiongea alipohutubia mkutano wa muungano wa Afrika AU mjini Addisa Ababa nchini Ethiopia Ban amesema kuwa idara hizo ni lazima zionyeshe kuchukua hatua katika masuala kama vile uundaji wa katiba, katika mapatano, katika hutoaji wa huduma muhimu pamoja na katika usalama. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud