Haki za watu wa asili Australia zilindwe:Pillay

25 Mei 2011

Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay akizungumza mjini Canbera katika siku ya mwisho ya ziara yake nchini Australia amepongeza utamaduni wan chi hiyo lakini amesema amesikitishwa na mfumo wa serikali kushindwa kuyalinda baadhi ya makundi ya watu wa jamii zake.

Amesema masuala ya haki za watu wa asili na wanaoomba hifadhi yanapaswa kushughulikiwa na sio tuu kwa sababu za muda mfupi za uchaguzi wa kisiasa bali suluhu ya kudumu.

Hata hivyo amepongeza juhudi za serikali kushughulikia haki za watu wenye ulemavu, na haki za wazee.Na ametoa wito wa kuzishirikisha jamii za Aborigina katika masuala muhimu yanayohusu haki za jamii hizo.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

Kwa upande wa waoomba hifadhi amekosoa vikali jinsi wanavyotendea baada ya kuzuru mahabusu ya uhamiaji mjini Darwin.Amesema watu hao hususbiri hadi mwaka mzima kuweza kuahilia na huo ni ukiuaji wa haki za binadamu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud