Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban arejea wito kwa Libya kusitisha mapigano

Ban arejea wito kwa Libya kusitisha mapigano

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwa njia ya simu na waziri mkuu wa Libya Al Baghdad Ali Al- Mahmoudi. Amesema waziri mkuu huyo kwa mara nyingine ameelezea hofu yake juu ya mashambulizi ya anga ayanyoendeshwa na NATO nchini Libya.

Ban hata hivyo amerejea wito kwake kwa serikali ya Libya kuwa na muafaka wa kweli wa kusitisha mara moja mapigano na kuanza mara moja majadiliano ya yatakayozingatia matakwa na wananchi wa Libya.

Ban amemwambia waziri mkuu kwamba mwakilishi wake maalumu Abdel-Elah Ali-Khatib amekuwa na mazungumzo na upande wa upinzani alipozuru mjini Tripoli na atarejea tene nchini humo hivi karibuni.