Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya ya mama na mtoto itakuwa ajenda Ban akizuru mataifa manne wiki ijayo

Afya ya mama na mtoto itakuwa ajenda Ban akizuru mataifa manne wiki ijayo

Afya ya mama na mtoto itakuwa ni ajenda kuu wiki ijayo wakati Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon atakapozuru mataifa manne ambayo ni Ivory Coast, Nigeria, Ethiopia na Ufaransa.

Ziara yake nchini Nigeria na Ethiopia ni sehemu ya juhudi za kimataifa za kampeni ya kuchagiza afya ya mama na mtoto kampeni ijulikanayo kama “kila mama, kila mtoto” ambayo ilizinduliwa na Ban Ki-moon mwezi September mwaka jana wakati wa mkutano wa malengo ya maendeleo ya milenia kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)