Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni miaka 63 tangu nakba, machafuko yaliyosababishwa kukaliwa kwa Wapalestina:

Ni miaka 63 tangu nakba, machafuko yaliyosababishwa kukaliwa kwa Wapalestina:

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu kwa eneo la Wapalestina linalokaliwa Richard Falk ameadhimisha miaka 63 ya Nakba, ambayo ni mwanzo wa machafuko na mkasa kwa Wapalestina uliosababisha kupokonywa ardhi zao na kukaliwa.

Katika maadhimisho hayo bwana Falk amesema Nakba mwaka huu imeadhimishwa kwa kughubikwa na mauaji ya waandamanaji waliokuwa wakikumbuka siku ambayo himaya ya Palestina ilianza kukaliwa . Siku hiyo imekuwa ya umwagaji damu sio tuu kwa eneo la Palestina bali pia katika maeneo mengine ya kanda hiyo. George Njogopa anaripoti.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)