Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya 1800 wakimbia machafuko Colombia:UNHCR

Watu zaidi ya 1800 wakimbia machafuko Colombia:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linahofia ongezeko la watu wanaolazimika kukimbia nyumba zao hivi karibuni Magharibi mwa Colombia kufuatia machafuko.

UNHCR inasema katika miezi miwili iliyopita watu 1800 pwani ya Pacific katika maeneo ya Valle del Cauca, Cauca, Choco na Narino wamelazimika kwenda kutafuta hifadhi sehemu zingine zenye usalama kwa kuogopa kukumbwa na machafuko baina ya makundi haramu yenye silaha yanayogombea udhibiti wa machimbo ya madini na kilimo cha coca.

Mwezi huu pekee watu 200 walikimbia jamii ya Illano mjini Buenaventura huku mapigano kwenye mji wa Narino mpakani mwa Ecuador yamewafungisha virago watu zaidi ya 400 wakiwemo Wacolombia wenye asili ya Afrika na watu wa asili katika eneo hilo.