Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na washirika wamepongeza rais mpya wa Haiti

UM na washirika wamepongeza rais mpya wa Haiti

Umoja wa Mataifa na washirika wake wamempongeza rais mpya wa Haiti Michel Martelly kwa kuibuka mshindi kwenye uchaguzi wa urais wakisema kuwa wako tayari kushirikiana na utawala wake mara utakapo apishwa.

Ujumbe wa Umoja wa Mataiafa ulio na wajibu wa kuleta utulivu nchini Haiti wa MINUSTAH unasema kuwa umemuunga mkono rais Martelly anapojiandaa kuongoza nchi hiyo katika siku za baadaye. Matamshi hayo ni ishara ya kujitolea kwa Umoja wa Mataifa katika kuunga mkono uamuzi wa wananchi wa Haiti katika kuwachagua viongozi wao kwa njia ya haki na usawa.

Pia umetoa wito kwa pande zote za kisiasa kuwa watulivu hasa kufuatia madai ya kuwepo kwa na dosari kwenye makaratasi ya kupigia hali iliyozua maswali mengi kuhusu uwazi kwenye uchaguzi huo.