Skip to main content

Kuuawa kwa magaidi sio dawa ya ugaidi

Kuuawa kwa magaidi sio dawa ya ugaidi

Mkutano unaojadili njia za kuzuia na kupambana na ugaidi unaendelea mjini Strasbourg nchini Ufaransa ambapo masuala kadha yanohusu njia za kupambana na ugaidi yanajadiliwa na baraza la ulaya na kamati ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidi.

Ekmeleedin Ihsanoglu katibu mkuu wa mkutano huo wa kiislamu amesema kuwa kuwaua magaidi hakutamaliza ugaidi.

Amesema kuwa ni lazima kuwe na suluhu la dunia nzima akiongeza kuwa zaidi ya dola trilioni moja zimetumika katika kile kijulikanacho kama vita dhidi ya ugaidi lakini hata hivyo matokeo yake ni yale hayakutarajiwa.