Wapiganaji wa zamani Sudan Kusini warejea uraiani

Wapiganaji wa zamani Sudan Kusini warejea uraiani

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linawasaidia wapiganaji wa zamani Sudan Kusini kurejea maisha ya kawaida wakati eneo hilo linapojiandaa kuadhimisha uhuru wake mwezi Juni mwaka huu kufuatia kura ya maoni iliyofanyika mapema mwaka huu.

IOM inalenga kuwabadili wapiganaji wa zamani 10,000 katika majimbo matano kwa ushirikiano na serikali ya Sudan Kusini , mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan. George Njogopa anaarifu.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Tangu mwaka 2005 shirika hili la wahamiaji IOM limeendesha mkakati wa kuyarejesha kwenye jamii ya kawaida makundi ya watu waliotumikia vikundi vya waasi na inadariwa kwamba zaidi ya watu 510,000 wamefaidika na mpango huo ambao sasa wamechangamana na jamii ya kawaida.

Shabaya kubwa ya mpango huu ni kuwajumuisha kwenye jamii ya kawaida askari wa zamani walijitumbukiza kwenye vikundi vya waasi, na kufanikisha azma hiyo watu hao ikiwemo wanawake ambao huendelezwa kwa njia mbalimbali ili baadaye waweze kushiriki kwenye shughuli za uzalishaji mali.

IOM imetumia kiasi cha dola za kimarekani milioni 8.8 katika kipindi cha kuanzia June 2010 kuteleza mradi huo unaofahamika kama DDR na imepanga kuendelea tena hadi Agusti mwaka huu 2011.