Skip to main content

Hii ni fursa ya mwisho kwa Gbagbo kuondoka:Ban D.C

Hii ni fursa ya mwisho kwa Gbagbo kuondoka:Ban D.C

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amesema Umoja wa mataifa kila siku unafanya mambo ambayo hakuna nchi yoyote inaweza kufanya peke yake.

Ban ameyasema hayo mjini Washington , D.C ambako amekutana na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton na wajumbe wengine wa ngazi ya juu wa kamati ya wizara ya mambo ya nje . Katika mkutano wao wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo hali inayoendelea Ivory Coast na Libya, na pia maeneo mengine yenye matatizo hivi sasa ambako Umoja wa Mataifa umechukua jukumu kubwa.

Ban amewaambia wajumbe wa wizara ya mambo ya nje kwamba kwa Laurent Gbagbo wa Ivory Coast hii ni fursa yake ya mwisho kuondoka ameongeza kuwa ni lazima azingatie maslahi ya watu na taifa lake, usalama na matarajio ya nchi hiyo.

Ameongeza kuwa Umoja wa Mataifa kwa kila njia unafanya mambo mengi kila siku ambayo hayawezi kufanywa na nchi yoyote.