Skip to main content

Msimamo wa itikadi kali za kidini ukomeshwe:Sampaio

Msimamo wa itikadi kali za kidini ukomeshwe:Sampaio

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye muungano wa ustaarabu Jorge Sampaio ameushauri ulimwengi kuwa na uvumilibu na kukoma kuendesha siasa kali.

Rais huyo wa zamani wa Ureno amesema kuwa matamshi pamoja na vitendo vya hivi majuzi vya muhubiri Terry Jones ni hatari na vinaonyesha ukosefu wa heshima kwa dini ya kiislamu. Amesema kuwa kuikufuru Koran takatifu ni kitendo kinachostahili kulaaniwa .

Matamshi ya bwana Sampaio yanajiri baada ya maandamano ya siku ya Ijumaa nchini Afghanistan ambapo waandamanaji waliokuwa wakipinga kuchomwa kwa Koran na mhubiri Terry Jones kutoka Marekani waliingia kwenye makao ya Umoja wa Mataifa na kuwaua wafanyikazi saba .

Sampaio amesema kuwa chuki miongoni mwa dini ambayo husababisha kutokea kwa ghasia na kuwashambulia wahumini ni lazima ilaaniwe na kuzuiwa.