Skip to main content

Ukiukwaji wa haki za binadamu unatendeka Ivory Coast:UM

Ukiukwaji wa haki za binadamu unatendeka Ivory Coast:UM

Wakati mapigano yakizidi kuchacha nchini Ivory Coast Umoja wa Mataifa unasema kuwa pande husika zinaendesha ukiukwaji wa haki za binadamu kila ujao.

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa anasema wanaripoti kuwa vikosi vinavyomuunga mkono rais Alassane Ouattara vimekuwa vikitekeleza vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilipokuwa vikielekea mji wa Abidjan.

Navyo vikosi vinavyo muunga mkono Laurent Gbabo vinaripotiwa kuwaua kinyama raia wawili na kufyatua makombora kwenda kwa maeneo wanamoishi raia mjini Abidjan. Rupert Colville ni kutoka afisi ya shirika la kulinda haki za binadamu la Umoja wa Mataifa

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Anasema kuwa baadhi ya vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyoendesha ni pamoja na uporaji , utekaji nyara , kuwakamata watu na dhuluma zingine dhidi ya raia.