Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNODC yazungumzia umuhimu wa Kenya katika usalama

UNODC yazungumzia umuhimu wa Kenya katika usalama

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na madawa ya kulevya pamoja na uhalifu UNODC Yury Fedotov hii leo amefanya mikutano na maafisa wa serikali ya Kenya kujadili shughuli zinazoendelea katika eneo hilo.

Bwana Fedotov amesema kuwa Kenya ina wajibu muhimu katika kanda ya Afrika Mashariki na kwamba ni mshirika mkubwa katika kupambana na vitendo vilivyo hatari kwenye usalama wa eneo hilo na wa kimataifa.

Ziara ya Fedotov inaambatana na mikutano kadha na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambapo pia atatambelea gereza la Shimo la Tewa mjini Mombasa kama moja ya mikakati ya shirika hilo ya kukabiliana na uharamia. Shirika hilo pia limekuwa likishirikiana pakubwa na serikali ya Kenya kwenye masuala ya mabadiliko kwenye idara ya polisi.