Skip to main content

UNAMID yafuatilia kwa karibu taarifa ya kitisho toka Minny Minnawi

UNAMID yafuatilia kwa karibu taarifa ya kitisho toka Minny Minnawi

Muungano wa vikosi vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika ambavyo vinaendesha operesheni ya amani huko Darfur UNAMID, umesema umechukua kwa uzito mkubwa taarifa ya hivi karibuni ya kiongozi wa kundi la waasi aliyedai kuwepo kwa kusudio la kufanya mashambulizi katika sehemu kadhaa muhimu kwenye eneo hilo.

Katika taarifa yake hivi karibuni, kiongozi wa kundi la Sudan Liberation Army Minny Minnawi alionya kuwa maeneo ya viwanja vya ndege vya Sudan, na maeneo kadhaa ya Darfur yamelengwa na kundi lake kwa ajili ya kufanyiwa mashambulizi ya kijeshi

 

Pia taarifa hiyo ilizionya taasisi za kimataifa pamoja na UNAMID kutotumia viwanja vyovyote vya ndege kwa wakati huu kwani wanaweza kutumbukia kwenye mashambulizi hayo. Alice Kariuki na taarifa kamali:

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)