Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya UM kufanya ziara Urusi

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya UM kufanya ziara Urusi

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini Urusi na mji St. Petersburg mwezi huu kama moja ya njia ya kuboresha uhusiano na Urusi katika masuala ya haki za binadamu.

Pillay anatarajiwa kukutana na rais wa Urusi Dmitry Medvedev na mawaziri kadha, wanasheria pamoja na mahakimu. Ziara hiyo itang'oa mnamo tarehe 13 mwezi huu na kumalizikia kwenye mji wa St. Petersburg tarehe 19. Akiendelea na ziara hiyo ambayo unakuja kwa mwaliko wa urusi Pillay anatarajiwa kuzungumzia masuala kadha na utawala wa Urusi ambapo pia atakutana na mkuu wa mahakama ya kikatiba na mkuu wa tume ya haki za binadamu. Pillay pia atatoa hotuba kwenye vituo vya PFUR na MGIMO ikiwa ndiyo ziara yake ya kwanza nchini Urusi kama mkuu wa tume ya haki za binadamu ya umoja wa mataiafa