Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha Urusi kuidhinisha mkataba wa nyuklia

Ban akaribisha Urusi kuidhinisha mkataba wa nyuklia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataiofa Ban Ki moon amekaribisha hatua ya bunge la Urusi ya kupitisha sheria ya kuidhinisha mkataba wa kupunguza zana za kinyuklia iliyouitia sahihi mwaka uliopita na Marekani hatua ambayo umeufanya mkataba huo kuanza kutekelezwa.

Mkataba huo mpya ujulikanao kama (New START Treaty) ulitiwa sahihi na rais wa Marekani Barack Obama pamoja na rais wa Urusi Dmitry Medvedev mwezi Aprili mwaka uliopita .Hatua hiyo ya Urusi inajiri baada ya bunge la Marekani kuchukua hatua kama hiyo mwezi uliopita ya kuuidhinisha mkataba huo.

Kupitia kwa msemaji wake Ban anasema kuwa ana matumaini kuwa urusi na Marekni watashirikiana ili kuhakikisha kuwa wamepunguza kila aina ya zana za kinyukia baada ya kukubaliana kupunguza zana zao za kinyuklia wa thuluthi moja.