Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika na jumuiya ya kimataifa iunge mkono matakwa ya Wasudan:Tanzania

Afrika na jumuiya ya kimataifa iunge mkono matakwa ya Wasudan:Tanzania

Serikali ya Tanzania imezitaka nchi zingine za Afrika na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla kuheshimu matakwa ya watu wa Sudan ambao wanapiga kura ya maoni hivi sasa kuamua endapo Sudan Kusini ijitenge na kuwa taifa huru mala la.

Kauli hiyo imetolewa leo na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bernard Membe wakati alipokutana na mabalozi wa Afrika na wa nchi za Magharibi jijini Dar es salaam.

Membe amekutana na watu hao kuzungumzia msimamo wa Tanzania kuhusu kura ya maoni ya Sudan Kusini na mvutano wa madaraka unaoendelea nchini Ivory Coast. George Njogopa na ripoti kamili kutoka Dar es salaam Tanzania.