Muafaka wa masuala ya silaha Nepal lazima upatikane:UM

10 Januari 2011

Zikiwa zimesalia siku tano tuu kabla ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Nepal UNMIN kumaliza muda wake, mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo amerejea wito kwa pande zote husika katika mchakato wa amani kufikia muafaka wa suala muhimu la kufuatilia silaha na majeshi yaliyo na silaha baada ya mpango wa Umoja wa Mataifa kuondoka.

Akizungumza katika mkuutano wake wa mwisho na waandishi wa habari mjini Kathmandu mwakilishi huyo Karin Landgren amesema hata katika siku hizi za mwisho bado anamatumaini kwamba pande zote zitatafuta njia ya kutatua suala hilo.

UNIMIN ilianzishwa mwaka 2007 baada ya serikali na wanamgambo wanaofuata siasa za Kimao kufikia makubaliano ya amani na kumaliza vita vilivyokatili maisha ya watu 13,000. Bi Ladgren wiki iliyopita aliliambia baraza la usalama kwamba kumekuwa na hatua kidogo zilizopigwa katika masuala muhimu ya kuunda serikali mpya na kuwajumuisha waasi wa zamani 19,000 wanaofuata siasa za Kimao, pia katika kuundwa kwa mswada wa katiba mpya.

Amesema wakati UNMIN ikikaribia kuondoka pande husika nchi humo hazijakubaliana jnjia ya kufuatilia masuala ya silaha. UNMIN itamaliza rasmi muda wake Jumamosi ya wiki hii.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter