Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumapili Januari 9 huenda historia ikaandikwa, Sudan Kusini likawa taifa la 54 Afrika

Jumapili Januari 9 huenda historia ikaandikwa, Sudan Kusini likawa taifa la 54 Afrika

Wasudan Kusini wapatao milioni 4 wanatarajiwa kujitokeza Jumapili Januari 9 hadi 15 ili kufanya maamuzi yatakayobadili maisha yao daima.

Watapiga kura ya maoni kuamua endapo Sudan Kusini ijitenge na Kaskazini na kuwa taiofa huru ala la, na ikiamua kujitenga basi itaandika historian a kuongeza idadi ya mataifa ya Afrika ambapo taifa huru la Sudan Kusini litakuwa la 54.

Uamuzi wa kura hii umefikiwa baada ya maafikiano ya amani yliyotiwa saini mwaka 2005 yanayojulikana kama CPA. Miongoni na vipengee muhimu katika mkataba huo ni kura ya maoni ya Sudan Kusini na jimbo la utajiri wa mafuta la Abyei. Sudan Kusini na Kaskazini kabla ya kufikia hatua hii wamekuwa katika vita kwa miongo kadhaa