Kipindupindu chaua zaidi ya 2700 Haiti:OCHA

30 Disemba 2010

Watu 2700 wamefariki dunia kwa kipundupindu nchini Haiti kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA.

Shirika hilo libnasema watu wengine 70,800 wamelazwa hospitali baada ya kuambukizwa ugonjwa huo. OCHA imearifu ongezeko la visa na vifo vya kipindupindu katika eneo la Kusini na Mashariki mwa nchi hiyo.

Katika maeneo mengine hata hivyo maambukizi ya ugonjwa huo yamepungua tangu mwanzoni mwa mwezi huu. Shirika la afya kwa nchi za Amerika PAHO na shirika la afya duniani WHO wanaendelea kutoa msaada kuchagiza masuala ya afya na usafi katika nchi hiyo ya visiwa vya Carebbean.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter