Hali ya Afghanistan inaweza kuwa mbaya kabla ya kutengamaa:UM

Hali ya Afghanistan inaweza kuwa mbaya kabla ya kutengamaa:UM

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameonya kwamba wapigaji wa Afghanistan Taliban wanaweza kuanzisha mkakati mpya wa kuzusha mashambulizi mapya katika kipindi cha wiki chache zijazo.

Maafisa hao wamesema kuwa, Taliban inaweza kuchukua mkondo huo kama mbinu ya kufifisha juhudi zilizofikiwa na jumuiya za kimataifa nchini humo ambazo zimeweza kuleta utengamao mkubwa kwa baadhi ya maeneo.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo hilo Staffan de Mistura ameliambia baraza la usalama kuwa pamoja na changamoto za hapa na pale, lakini nuru njema imeanza kuchomoza nchini Afghanistan hatua ambayo inaweza kufungua milango ya kuanzisha meza mpya ya majadiliano kwa makundi yote hasimu. Amesifu uchaguzi uliofanyika hivi karibuni ambao amesema umefungua milango mipya ya kisiasa.