Skip to main content

UM walaani kufyatuliwa kwa makombora kwenda Israel

UM walaani kufyatuliwa kwa makombora kwenda Israel

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika eneo la mashariki ya kati amelaani mashambulizi ya makombora kwenda Israel na makundi ya wanamgambo kutoka ukanda wa Gaza.

Robert Serry amesema kuwa mashambulizi haya ambayo yameongezeka katika siku za hivi majuzi yanakiuka sheria za kibinadau za kimataifa na yanahatarisha maisha ya raia nchini Israel. Serry amesema kuwa Israel ina haki ya kujikinga kulingana na sheria za kimatiafa lakini wakati huo huo ameitaka Israel kujihadhari na kuhakikisha kuwa vikosi vyake havihatarishi maisha ya raia katika ukanda wa Gaza.

Naye mratibu wa masula ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi ya Palestina inayokaliwa na Israel Maxwell Gaylard ametembelea nyumba mashariki mwa mji wa Jerusalem ambazo Israel imetoa amri ya kubomolewa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekaribisha kura ya bunge la Marekani ya kuunga mkono kuidhinishwa kwa mkataba wa kupunguza zana za nyuklia uliotiwa sahihi mapema mwaka huu kati ya viongoiz wa Urusi na Marekani.