Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bangladesh na IOM kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu

Bangladesh na IOM kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu

Bangladesh mbioni kuanzisha sheria ya kukabiliana na biashara ya usafirishaji haramu wa binadamu

Bangladesh imeanzisha kipengele cha awali cha sheria yenye lengo la kukabiliana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu.

Katika mpango huo mpya, Wizara ya mambo ya ndani inashirikiana na mashirika kadhaa ya kirai kwa ajili ya kuandaa sheria ambayo itatumika kuwabana wahusika wa biashara hiyo. Tayari mkakati huo umewasilishwa kwa shirika la uhamiaji la umoja wa mataifa ambalo linatazamia kutoa mchango mkubwa kufanikisha sheria hiyo.

Vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu vimekuwa vikiongezeka kila mara nchini Bangladesh. Wengi wanaotumbukia kwenye hali hiyo ni wale wanaozamia katika nchi za majuu kwa ajili ya kusaka ajira. Mwaka jana 2009 pekeee watu zaidi 900,000 waliondoka nchini humo kwenda nchi za nje kwa shabaya ya kusaka kazi.