Skip to main content

Wazimbabwe walioko nje ya nchi kuhesabiwa na IOM

Wazimbabwe walioko nje ya nchi kuhesabiwa na IOM

Idara ya kitaifa inayohusika na takwimu nchini Zimbabwe kwa ushirikiano na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM imeandaa warsha ya kujadili changamoto za kuwatafuta walipo raia wake wanaoishi nchi za kigeni kabla ya zoezi la kitaifa la kuwahesabu watu linalotarajiwa kundaliwa mwaka 2012.

Warsha hiyo inayofadhiliwa na IOM na jumuiya ya ulaya imewaleta pamoja waakilishi kutoka wizara za serikali , viuo vikuu na mashirika mengine ya kimataifa kujadili mbinu za kupata idadi ya wazimbabwe wanaoishi mataifa ya kigeni. Kwa muongo mmoja uliopita Zimbabwe imeshuhudia misukosuko ya kiuchumi na kijamii ambayo imechochea watu kuihama nchi hiyo.

Kutokana na uhaba wa raslimali Zimbabwe haiukuwa na uwezo wa kufuatilia na kuweka takwimu za uhamajia kwa wanannchi wake hali ambayo imeifanya vigumu kufahamu idadi ya wananchi wake walio mataifa ya kigeni.