Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto 10,000 wana kipindupindu Haiti:WHO

Watoto 10,000 wana kipindupindu Haiti:WHO

Watoto takribani 10,000 wa chini ya umri wa miaka mitano wameambukizwa kipindupindu nchini Haiti limesema shirika la afya duniani WHO huku wengine 130 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

WHO inasema ingawa idadi ya waathirika wa kipundupindu inaendelea kuongezeka, idadi ya wanaokufa kutokana na ugonjwa huo inapungua. Takwimu za karibuni zinaonyesha kwamba visa 84,391 vimeripotiwa na waliofariki dunia hadi sasa ni 1882.

Dr Erick Laroche kutoka WHO anasema mlipuko wa kipindupindu nchini Haiti unaweza kudumu hadi miazi 12. Anasema usalama mdogo na mfumo mbaya wa barabara nchini humo vimekuwa vikwazo vya kuwafikia watu wa vijijini ambako kasi ya maambukizi ni kubwa.

(SAUTI YA DR ERIC LAROCHE)

Ombi la dola milioni 164 limetolewa na Umoja wa Mataifa ili kusaidia kugharamia matibabu ya kipindupindu na juhudi za kuzuaia. Hadi sasa kuna upungufu mkubwa wa fedha Haiti ambapo imepokea dola milioni 34 pekee.