Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bodi ya IAEA inajadili Iran, Syria na Korea ya Kaskazini.

Bodi ya IAEA inajadili Iran, Syria na Korea ya Kaskazini.

Bodi ya wakurigenzi wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA leo limeanza mkutano mjini Geneva kujadili masuala ya nyuklia yanayohusiana na Iran, Syria na jamuhuri ya Kidemokrasi ya watu wa Korea DPRK.

Katika hotuba ya ufunduzi wa mkutano huo mkurugenzi mkuu wa IAEA Yukiya Amano ameainisha mipango ya shirika hilo kwa mwaka 2011 akisisitiza afya za watu. Nchi wanajama barani Afrika, Asia, Pacific na Ulaya wanaonyesha hamasa ya kuwa na nguvu za nyuklia. Lakini amesema cha kusikitisha ni nchi kama DPRK ambazo haziko tayari kutoa ushirikiano kwa ukaguzi wa mitambo na vinu vyake vya nyuklia.

(SAUTI YA YUKIYA AMANO)