Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni muhimu kuongeza vikosi vya kulinda amani Somalia: Mahiga

Ni muhimu kuongeza vikosi vya kulinda amani Somalia: Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Somalia Balozi Augustine Mahiga anasema bila kuongeza vikosi hivyo na msaada wa kiufundi vita vya Somalia na hali ya usalama itaendeleo kuwa tete.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limejadili suala la Somalia ambapo hali ya usalama na vikosi vya kulinda amani vya muungano wa Afrika zimekuwa ajenda kuu.

Mwakilishi huyo pia amezungumzia umuhimu wa ziara ya Rais Yoweri Museveni wa Uganda mjini Moghadishu mwishoni mwa juma na kusema sio tuu kuwa imewatia motisha walinda amani wa AMISOM kutoka Uganda na Burundi bali pia imeonyesha nia ya nchi za Afrika kusaidia kumaliza tatizo la Somalia lililodumu kwa zaidi ya miongo miwili sasa. Anajadili masuala hayo na Flora Nducha ungana nao.