UM umelaani ghasia zilizotokea jana Haiti
Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUSTAH umelaani ghasia zilizozuka jana dhidi ya walinda amani wake wakati wa maandamano mjini Cap-Haitien na Hinche ukisema machafuko hayo yaliyosababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi wengine yalichochewa kisiasa.
MINUSTAH imewataka watu wa Haiti kutulia na kutokubali kudanganywa na maadui wa amani , utulivu na demokrasia nchini humo.Waliojeruhiwa ni pamoja na wafanyakazi sita wa MINUSTAH. Wakati huohuo mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa aynaendelea kuwasaidia waathirika wa kipundupindu na kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.
Shirika la afya duniani WHO limesema ingawa kujua chanzo cha ugonjwa huo ni muhimu na uchunguzi unaendelea lakini kwa sasa cha kuzingatia ni kutoa matibabu kwa waathirika na kutoa elimu ya kuzuaia kusambaa kwa ugonjwa huo, kama anavyofafanua Fadela Chaib wa shirika hilo.
(SAUTI YA FADELA CHAIB)