Zaidi ya watu 400 wahusishwa na kundi la Al-Qaeda

Zaidi ya watu 400 wahusishwa na kundi la Al-Qaeda

Mwenyeketi wa kamati ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa inayohusika na vikwazo dhidi ya makundi ya kigaidi amesema kuwa kuna zaidi ya watu 400 walio na uhusiano na makundi ya kigaidi ya Al-Qaeda na Taliban.

Akilihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo Thomas Mayr-Harting amesema kuwa kamati yake ilikamilisha uchunguzi wake tarehe 29 mwezi Julai mwaka huu. Amesema kuwa kati ya majina 488 yaliyokaguliwa majina 45 yaliondolewa kutoka kwenye orodha hiyo. Ameongeza kuwa majina 58 yaliyowasilishwa mbele yake wakati wa ukaguzi wa majina mengine yatachunguzwa badaye na kamati hiyo.