Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto milioni 134 kuchanjwa surua India:UNICEF

Watoto milioni 134 kuchanjwa surua India:UNICEF

Shughuli ya kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa kwa Surua nchini India inayofadhiliwa na shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na lile la afya duniani WHO imeng\'oa nanga

Mwakilishi wa shirika la UNICEF nchini India Karin Hulshof anasema kuwa awamu ya pili ya kutoa chanjo inahakikisha kuwa wale walioikosa awali wameipata ili kuwalinda kutokana na ugonjwa huu hatari. Ugonjwa wa Surua ni kati ya magonjwa hatari zaidi duniani na moja ya magonjwa yanayosababisha vifo vingi zaidi miongoni mwa watoto.