Hatua imepigwa katika kuleta amani maziwa makuu:Mulamula

5 Novemba 2010

kongamano la kimataifa la amani ya kanda ya maziwa makuu limesema lina matumaini ya amani zaidi.

Kongamano hilo linalojumuisha viongozi wa kikanda, jumuiya ya kimataifa, Umoja wa Mataifa, jumuiya za kijamii, muungano wa Afrika na wadau wa masuala ya amani linasema hatua kubwa imepigwa katika kustawisha masuala ya amani ya kanda hiyo iliyoshuhudia vita na machafuko kwa miongo kadhaa.

Jumuiya ya kanda ya maziwa makuu ina nchi 11 zinazozunguka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na ilianzishwa na jumuiya ya kimataifa mwaka 2004 baada ya migogoro ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Licha ya eneo hilo kuanza kupata nuru bado kuna changamoto kubwa hasa makundi ya waasi huko DR Congo na umasikini uliokithiri kama balozi Liberata Mulamula katibu mtendaji wa sekretariati ya kongamano la kimataifa la kanda ya maziwa makuu alivyomfahamisha mwandishi wetu Ramadhani Kibuga. Kwanza anafafanua nini kilikuwa ajenda.

(MAHOJIANO KIBUGA NA MULAMULA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter