Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kipindupindu huenda kikasambaa Port au Prince:WHO

Kipindupindu huenda kikasambaa Port au Prince:WHO

Shirika la afya duniani WHO linasema kuna hofu kwamba mlipuko wa kipindupindu nchini Haiti huenda ukasambaa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Port au Prince.

Visa vitano tayari vishaarifiwa Port au Prince na vingine vingi vinachunguzwa. Fadela Chaib wa WHO anasema asilimia 75 ya walioathirika na ogonjwa huo hawaonyeshi dalili zozote, lakini wanaweza kuzagaza bacteria wa ogonjwa huo wiki mbili baada ya kuathirika na kuweza kuwaambukiza wengine. Hata hivyo amesema hakuna haja ya hofu hiyo kusababisha mipaka ya Haiti kufungwa.

(SAUTI YA FADELA CHAIB)

Kipundupindu nchini Haiti hadi sasa kimeshauwa watu 259. Wakati mashirika ya Umoja wa Mataifa yakizidisha usambazaji wa madawa, kampeni kubwa ya kuielimisha jamii pia inaendelea ikiwataka kutumia maji safi, kuwa wasafi na kuwa waangalifu na vyakula, ikiwemo kunawa mikono na kuzuia kusambaza vinyesi katika maeneo ya wazi.